Mazungumzo baina ya Mratibu wa SOMAIT na Mkuu wa Kitengo cha Habari Baraza la Mji Kati, Zanzibar

  • 11 August, 2025
Mazungumzo baina ya Mratibu wa SOMAIT na Mkuu wa Kitengo cha Habari Baraza la Mji Kati, Zanzibar

Jumapili Agosti 10, 2025, Mratibu wa SomaIT Institute Of Technology, Ahmed Rashid alipata fursa ya kutembelea Maonesho ya 88 ya Nanenane yanayoendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Dole, Kizimbani, kisiwani Unguja.

Maonesho ya Nanenane ni sikukuu kubwa. Ni tukio kubwa linalowakutanisha pamoja wakulima, wafugaji, wavuvi, taasisi za fedha, wabunifu wa teknolojia na wadau wa sekta ya kilimo kutoka kila kona ya Tanzania na nje ya nchi.

SomaIT ni taasisi ya teknolojia na moja ya shabaha zake ni kuleta mapinduzi ya kidijitali nchini na kusaidia juhudi za serikali za kufanikisha malengo yake ya muda mrefu.

Katika kutembelea maonesho hayo, Mratibu wa SomaIT alipata fursa ya kukutana, kujadiliana na kubadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Habari Baraza la Mji Kati, Bi Fatma Ali Said ili kujua ni katika nyuga gani SomaIT inaweza kushirikiana na Baraza la Mji Kati kusaidia jitihada za Serikali za kufanikisha malengo yake.

Miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa kwenye mazungumzo hayo ni kutiwa nguvu wafanyakazi wa Baraza la Mji katika matumizi ya mawasiliano ya kompyuta na kukusanya data zao kidijitali na kuondokana na mazoea ya kuhifadhi data kwenye mabuku ambayo mbali na usumbufu wake wa kuingiza data lakini pia kuna hatari kubwa ya kupotea data muhimu.

Sambamba na taarifa hii tumeweka baadhi ya picha za mazungumzo baina ya Mratibu wa SomaIT, Ahmed Rashid na Bi Fatma Ali Said, Mkuu wa Kitengo cha Habari Baraza la Mji Kati Zanzibar.

 

43 views
1 shares