Katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, Somait Institute of Technology linawakaribisha kwenye darasa maalum la Graphics Designing litakalofanyika hivi karibuni.
Katika kipindi cha miaka 61 ya Muungano wetu, teknolojia imekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha watu, kuboresha mawasiliano, na kuibua fursa mpya za ubunifu. Kupitia darasa hili, washiriki watapata nafasi ya kujifunza mbinu za kisasa za ubunifu wa kidigitali, wakijifunza jinsi maendeleo ya teknolojia yanavyoweza kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kwa vizazi vijavyo.
Usikose fursa hii adhimu ya kuongeza maarifa yako ya kidigitali!
Ikiwa unataka kuwa mtaalam wa masuala ya kompyuta na teknolojia, hii ni nafasi yako.
Jisajili sasa kupitia: https://somait.ac.tz/application
Au wasiliana nasi kwa simu: 0772 05 88 99.
Tarehe ya Tukio: 27/04/2025
Mahali: Somait Institute of Technology, Kwa Bakathiri, Kiembe Samaki, Unguja
Karibu tujifunze, tuhamasike, na tuendelee kuijenga Tanzania yetu kupitia ubunifu wa kidigitali!